This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday, November 22, 2016

KILIMO DIJITALI NA SHERIA ZAKE


Baada ya kuona taarifa na matangazo mengi yanayohusu faida za kilimo na uzuri wa kipato chake, nilitamani kupata kujua hasa mtu wa kawaida (kama mimi) nisiyekuwa na ujuzi katika kilimo ningeweza vipi kupata taarifa za jinsi gani nitaweza kujihusisha pia na kilimo. Kwa uzuri wa mitandao nikaona nisipoteze muda, nianze kujifunza yale niwezayo katika muda niliokuwa nao ili kama ikiwezekana nianze kujifunza kidogo kidogo.
Siku moja rafiki yangu (kutoka grupu moja la whatsap) alishea ishu moja na picha zinazohusiana na kilimo, na mimi bila kuzuga nikamuinboksi kumuulizia kama ana chochote angeweza nielekeza juu ya aina ya kilimo alichokuwa akikifanya. Naye hakuwa mchoyo, akaniomba tukuane ili anipe somo Zaidi.
Wiki iliyofuata nikajibeba na kumfuata katika ofisi yake moja iliyopo karibu kidogo ya katikati ya mji (Mwenge pale), nikakutana naye, tukapiga stori, na akanitisha vya kutosha juu ya makosa ambayo wakulima wengi wanaoanza na walio katika hali kama yangu hupitia ambayo mwishoni huwakosesha kiasi cha mazao na faida wanazozitegemea. Pia akaniasa kuwa kilimo ni MOYO na UTAYARI, sio kwamba element ya biashara, uongozi na faida havihusiki, ila Zaidi ni moyo wa uvumilivu na akili ya utayari wa kujifunza ndivyo humfanya mkulima awe bora na kumfanya apate matokeo anayostahili.
Pia rafiki yangu huyo aliyetoka kupata mazao mengi sana msimu ule aliniambia kuhusiana na kilimo dijitali na sharia zake ambazo wakulima wengi huzidharau na kuziona ni za kuzipuuza. Baadhi ya sharia hizo za kilimo dijitali ni;
  • Shamba halilimwi kwa simu
  • Kabla ya kugusa udongo ni muhimu kuufahamu, na kama ikiwezekana kuupima
  • Gharama nyingi za kwenye makaratasi SIO gharama halisi za ardhini
  • Jinsi ya kumroga mfanyakazi (kibarua wako) kidijitali
  • Ratiba nzima ya shambani, siku ya kwanza hadi ya mwisho.

·         Mengine mengi yanayokwenda mpaka maishani baada ya kutoka shambani

Mengi ya sharia hizi tutaendelea kushea kwa undani Kadri tunavyozidi kuingia kilimoni, ila kwa kuanzia hizi ndizo zilikuwa za muhimu zaidi