Baada ya kuona taarifa na matangazo mengi yanayohusu faida
za kilimo na uzuri wa kipato chake, nilitamani kupata kujua hasa mtu wa kawaida
(kama mimi) nisiyekuwa na ujuzi katika kilimo ningeweza vipi kupata taarifa za
jinsi gani nitaweza kujihusisha pia na kilimo. Kwa uzuri wa mitandao nikaona
nisipoteze muda, nianze kujifunza yale niwezayo katika muda niliokuwa nao ili
kama ikiwezekana nianze kujifunza kidogo kidogo.
Siku moja rafiki yangu (kutoka grupu moja la whatsap)
alishea ishu moja na picha zinazohusiana na kilimo, na mimi bila kuzuga
nikamuinboksi kumuulizia kama ana chochote angeweza nielekeza juu ya aina ya
kilimo alichokuwa akikifanya. Naye hakuwa mchoyo, akaniomba tukuane ili anipe
somo Zaidi.
Wiki iliyofuata nikajibeba na kumfuata katika ofisi yake
moja iliyopo karibu kidogo ya katikati ya mji (Mwenge pale), nikakutana naye,
tukapiga stori, na akanitisha vya kutosha juu ya makosa ambayo wakulima wengi
wanaoanza na walio katika hali kama yangu hupitia ambayo mwishoni huwakosesha
kiasi cha mazao na faida wanazozitegemea. Pia akaniasa kuwa kilimo ni MOYO na UTAYARI,
sio kwamba element ya biashara, uongozi na faida havihusiki, ila Zaidi ni moyo
wa uvumilivu na akili ya utayari wa kujifunza ndivyo humfanya mkulima awe bora
na kumfanya apate matokeo anayostahili.
Pia rafiki yangu huyo aliyetoka kupata mazao mengi sana
msimu ule aliniambia kuhusiana na kilimo dijitali na sharia zake ambazo wakulima
wengi huzidharau na kuziona ni za kuzipuuza. Baadhi ya sharia hizo za kilimo
dijitali ni;
- Shamba halilimwi kwa simu
- Kabla ya kugusa udongo ni muhimu kuufahamu, na kama ikiwezekana kuupima
- Gharama nyingi za kwenye makaratasi SIO gharama halisi za ardhini
- Jinsi ya kumroga mfanyakazi (kibarua wako) kidijitali
- Ratiba nzima ya shambani, siku ya kwanza hadi ya mwisho.
·
Mengine mengi yanayokwenda mpaka maishani baada
ya kutoka shambani
Mengi ya sharia hizi tutaendelea kushea kwa undani Kadri tunavyozidi
kuingia kilimoni, ila kwa kuanzia hizi ndizo zilikuwa za muhimu zaidi
0 comments:
Post a Comment