Wednesday, December 21, 2016

PANYA na FUKO SHAMBANI


JINSI YA KUPAMBANA na PANYA & FUKO SHAMBANIπŸ€ 

πŸ•³Kwanza kabisa tufaham kuwa PANYA na FUKO ni wanyama waharibifu sana shambani  kama walivyo wanyama wengne waharibuo mazao shambani..
    πŸ‰ Leo nimesikitika sana kuna rafki yang kakutana na changamoto ya panya kuharibu TIKITI lake shamban, tikiti ambalo limeshaanza kukomaa.
    πŸ€ Hivyo nikaona si vyema kama sinto-share nanyi kuwa ni jinsi gani ambavyo tunaweza kupambana na wanyama hawa waharibifu MAANA wengi mmekua mkihangaika kumalizana na hawa jamaa..Na hii ndiyo komesha yao, Twenden..!

CHANGANYA MCHANGANYIKO HUU VIZURIπŸ‘‡

  • Cement - 3kg
  • Unga wa ngano -1kg  
  • Dagaa waliosagwa -robo
  • Unga wa cocoa -vijiko 6
  • Chumvi laini -vijiko 10  

  ⚗ Mchanganyiko utategemea na ukubwa wa vita yako .Kisha nenda maeneo wanayopenda kushinda au ficho lao mwaga mchanganyiko huu  halfu pembeni weka maji ya kunywa. LAKINI pia si lazima kutafuta maficho yao we tandaza tu kuzunguka shamba lako.


INAFANYAJE KAZI?

Mchanganyiko huu ni mtamu sana kwa PANYA/FUKO ,baada ya kufurahia mlo huu panya atasikia kiu kali ataenda kunywa maji,lahaula! atakuwa amekamilisha mchanganyiko wa kutengeneza kitofari chakum'bana tumbo ambacho kitamuua..😫

Mchanganyiko huu unauwezo wa kuua PANYA au FUKO 1000 ndani ya siku 3.

ANGALIZO:Wapo watu wanaoshauri kuweka sumu zile za viwandan ..skatai zile ni sumu nzuri kwa kupambana na panya LAKINI tukumbuke kuwa kwa sumu zile panya akiwahi kunywa maji anaweza kuendelea kuishi, hvyo kwa shamban sidhan kama sumu zile zitaweza kufanya kazi vizuri kwan shambani tumezungukwa na visima vya maji, lakin kwa mchanganyiko huu panya anywe maji asinywe lazima chamoto akipate..tena akinywa maji ndio anazidi kutengeneza zege zuri tumboni.

HIVYO KWA WALE WAKULIMA na PIA WALE WANAOSUMBULIWA na Panya majumbani mchanganiko huu ndio kiboko yao..

✍ na Mtaalamu:πŸ•΅πŸ»A.Aldinah

1 comments:

  1. Asante kwa maelezo yako.Naenda kufanyia majaribio na matokeo yake nitakujulisha.

    ReplyDelete